Katika Jarida la Habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea -Jawabu la maandamano ya kila kona duniani, ni kutokuwepo na uswwa na dawa pekee ni kuziba pengo hilo la usawa imesema Ripoti ya maendeleo ya binadamu ya UN iliyotolewa leo -Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema asilani hatoruhusu ufisadi ukwamishe ufikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs na kuzitaka nchi kuchukua hatua kupambana na jinamizi hilo