Hii leo Ijumaa katika muhtasari wa habari tunaanzia Nairobi Kenya kusikiliza manusura wa kuporomoka kwa jengo eneo la Embakasi kisha tunakwenda Karibea ambako mabadiliko ya tabianchi yazidi kuwa mwiba kwa watoto na huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wagonjwa wapya 9 wa Ebola wathibitishwa. Mada kwa kina leo ni mkutano wa 25 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP25 huko Hispania tumezungumza na Bwana Faizal Issa akiwakilisha taasisi ya Afrika. Ne neno la wiki hii leo ni Kwina! Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.